Simu za mkononi hutumia mionzi – rays – kuweza  kunasa mawimbi ya mtandao – waves. Mionzi hii hununurishwa kwenye simu muda wote – simu ikiwa imewaka – ili kutafuta mtandao. Mionzi hii ya simu si mizuri hata kidogo ikiingia kwenye mwili wa binadamu kwani husababisha madhara mengi kiafya – ikiwemo uwezekano wa kupata kansa ya ubongo na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Swala la kuogopa Zaidi ni kwamba madhara haya mionzi ya simu hayajitokei mapema. Inachukua muda, pengine mpaka mtu afikie umri wa kati kuanza kuona ama kugundua athari za mionzi ya simu. Hii ndio sababu ni vigumu watu kuchukua tahadhari kwa kuwa hawaoni athari za mapema ili wastuke.

Watafiti wanasema, kuna mabadiliko hutokea kwenye mishipa ya neva iliyo karibu nae neo la siko kabla na baada ya kuingia mionzi. Mishipa hiyo hubadilik rangi na kuwa nyekundu kabisa mara baada ya kukata simu. Hivyo kila unapopiga simu unaingiza kiwango Fulani cha mionzi kwenye ubongo wako.

Jinsi ya kuepuka

Unapoongea na simu kwa muda mrefu, tumia earphones au weka loudspeaker. Earphones zilizotengenezwa maalumu kwa simu hufanya kazi kama antenna hivyo kupunguza mionzi  inayotolewa na simu.

Epuka kuweka simu ndani ya mfuko wa suruali, shati au kwenye sidiria. Mionzi ya simu hupenya kwenye Ngozi, mifupa na pia kwenye nguo. Kama upo mazingira ya nyumbani tu huna haja ya kuweka simu mfukoni mwako.Pia unapopiga simu usiiweke moja kwa moja kwenye sikio, subiri mpaka ipokelewe.

Usitumie simu kwenye vyombo vya moto kama vile magari, ndege, meli n.k. mionzi ya simu huingiliwa/husumbuliwa na mifumo ya ki-elektroniki ya kwenye chombo cha moto – vehicle – hivyo, kuifanya simu itoe mionzi kwa nguvu Zaidi ili kuhimili usumbufu pamoja na ku-balance uwepo wa mtandao.

Mtoto mdogo asipewe simu. Fuvu la kichwa cha mtoto mdogo huwa bado linakua – plasticity – hivyo ni rahisi mionzi kupenya kwenye ubongo wake. Pia hata watoto chini ya umri wa miaka  kumi na nane wasipewe simu – labda kwa nadra sana.

Wakati wa kulala weka mbali simu. Usiweke chini yam to kwa maana utakuwa unaipa hali ngumu ya kutafuta mtandao badala yake mionzi inazalishwa kwa wingi. Ni vyema kuzima simu kabisa pale ambapo hautumii.

Usitumie simu kwenye majengo yaliyojengwa kwa bati au chuma tupu. Mionzi ya simu hupata shida kupenya katika vitu vizito kama vile chuma au bati. Mionzi kutoka kwenye simu hurudishwa kwenye simu nayo simu hutoa mionzi kwa wingi Zaidi ili kunsa mtandao – hii ni hatari zaidi.

Tumia simu ya mezani – landline. Ni rahisi kuepuka mionzi kwenye simu ya mezani kwa sababu ina waya hivyo utakaa mbali nayo wakati unaongea.