Katika mahusiano, kila mmoja wetu hupenda kuwa bora kwa mpenzi wake – inaweza isiwe bora kabisa lakini angalau kujitahidi kuonyesha kuwa unataka kuwa mtu aliye bora kwa mwenzi wako. Hii yote ni katika kutaka kudumisha mahusiano yenu. Unaweza kuwa mpenzi bora kwa kufanya mambo yafuatayo.

Kuwa muwazi

Usitegemee mwenzio agundue unachofikiria bali funguka – mueleze kile unachojisikia, mwambie kile  ambacho haukifurahii kutoka kwake na muombe ajaribu kurekebisha – epuka lugha za lawama na kukata tamaa.

Jenga amani ya kweli na si amani feki/uongo

Amani ya kweli itakusaidia kuona makossa na kuyatatua kwa faida ya wote. Usiwe na amani ya uongo – kwa mfano unaona kabisa mwenzio anakukosea halafu unaamuna kukaa kimya kwa kuogopa ukimwambia atachukia. Huko ni kutengeneza amani ya uongo wakati unaumia kwa ndani

Jenga Imani – kuwa mwenye kuaminika.

Mfanye mwenzio akuone wa kuaminika, usiwe muongo – mfano ukitoa ahadi jitahidi kuitekeleza hata kama si kwa muda muafaka aliotegemea. Usimfanye akuone mbabaishaji na mjanja mjanja asieyeaminika.

Thamini hisia za mwenzako

Usipuuzie hisia zake – jaribu kushughulikia mambo ambayo mpenzi wako anayapenda. Yawezekana mapendeleo ya mpenzi wako si sawa na yale wewe unayoyapenda – mfano mwenzako anapenda filamu za kikorea ilhali wewe unapenda filamu za Hollywood, basi jitahidi kuweka uwiano katika mapendeleo/interests yenu.

Kuwa msikilizaji mzuri

Jifunze kuwa msikilizaji mzuri – msikilize ili ugundue ndani mwake anawaza nini, msikilize na jitahidi kufanyia kazi anayokushauri. Wakati mwingine unaweza kuona mwenzako hakushirikishi mambo yanayo muhusu – anafanya hivyo kasababu anajua hata akikuambia huwa hausikilizi hivyo anaamua kuyaweka moyoni mwake tu.

Imarisha tendo la ndoa

Tendo la ndoa lifanyike katika hali ambayo kila mtu anafurahia na kuridhika – mshirikishe mwenzako katika kuimarisha madhaifu yanayojitokeza. Tendo la ndoa lifanyike katika hali ambayo mmoja asijione anatumiwa au kunyanyaswa – mwenzako akisema hajisikii basi heshimu maamuzi yake, mwenzako akikosa hamu jaribu kumsaidia kurejesha hamu.

Ongeza mbinu za kutatuta migogoro

Katika mahusiano migogoro haiepukiki – hivyo unatakiwa kuwa na mbinu za kuweza kuitatua migogor hiyo, mwenzako akinuna jaribu kuwa mbunifu kumfanya afurahi tena. Ni lazima uwe na nguvu ya kufuatilia na kutatua matatizo yote.