Biashara na matangazo ya karne ya 21 yanategemea sana teknolojia. Tunaishi ulimwengu wa dijiti hivyo kila kitu hakina budi kufanywa kidijitali. Unaweza kuwa na biashara yako au kampuni yako inayotoa huduma ama bidhaa imara na uhakika kabisa lakini usipotumia bidii kujitangaza unaweza kuzidiwa na watu ambao huduma zao hazina ubora zaidi yako.

Kujitangaza kimtandao ni njia rahisi na isiyo gharama kuwafikia watu wengi zaidi. Ukweli ni kwamba usipofanya matangazo ya biashara yako, yote uyafanyao yataishia kwa watu wachache tu wanaokuzunguka.

Nenda na wakati

Siku hizi mtu akitaka msaada wa jambo fulani wazo la kwanza kumjia ni kushika simu yake na kuperuzi kuhusu akitakacho. Hapo ndipo huweza kukutana na majibu ya swala alitakalo mtandaoni. Fikiria wewe ndiyo hauko mtandaoni, mtumiaji huyu wa simu atakufahamu vipi? Badilika. Nenda na wakati, hamia ulimwengu wa digitali. Wazungu wanaita ‘Digital Marketing’ mbinu ya kujitangaza kupitia tehama

Unaanzia wapi?

Ni rahisi. Ingawa  waweza kutumia pesa panapohitajika, kujitangaza mitandaoni ni bure kabisa. Ni kama vile ulivyo na akaunti facebook bilamalipo yoyote. Cha msingi ni wewe kujifunza mbinu za uendeshaji na kuchagua njia ipi inakufaa zaidi

Miliki tovuti yako

Tovuti hasa kwa mashirika, makampuni na biashara kubwa ni kitu cha lazima. Hii huongeza hadhi ya kampuni kwa ujumla. Tofauti kubwa kati ya tovuti ama website na mitandao mingine ya kijamii ni namna ya kuweka maudhui. Kupitia tovuti, mtu anaweza kupata taarifa kwa kina kuhusu kampuni au bidhaa. Pia kwenye tovuti kunaweza kufanyika shughuli kama manunuzi ya mtandaoni, kuandikisha watu kwa ajili ya program na kadhalika.

Unatengenezaje tovuti? Ni rahisi. Kuna makampuni kama HostBlast ambayo yapo kukusaidia kufungua tovuti yako kwa bei karibu na bure kabisa. unaweza kuwatembele HostBlast kujua zaidikuhusu kuanzisha tovuti yako kwa kubofya HAPA

Mitandao ya kijamii

Karibia kila mtu yuko Facebook au Instagram. Maana yake ni kwamba soko liko huko kwa sababu ndiko watu waliko. Cha kufanya ni kupeleka biashara yako huko. Fungua akaunti kwa jina la biashara au kampuni yako na uanze kujitangaza.

Nini cha kupost ukiwa huko? Hapa ndipo wengi hukosea. Akunti ya biashara inatakiwa iwe na muonekano kweli wa kibashara. Usichanganye mambo binafsi na biashara kwani utawachanganya wafatiliaji wako na pengine utaonekana hauko makini na ukifanyacho.

Unaweza ukawa unapost picha za bidhaa zako, picha za wateja wenye nyuso za kuridhika na huduma yako. Kama utakuwa mtundu zaidi waweza tengeneza vipande vifupi vya video. Kumbuka pia hautakiwi kupost mara kwa mara. Angalau mara nne kw wingi si mbaya, isipokuwa pale unapokuwa na matukio mfululizo na ni muhimu kuyaweka mtandaoni

Kuwa mbunifu katika uandishi

Karibia kila mtu anaandika maudhui mtandaoni. Iwe ni mstari mmoja kama status za facebook na whatsapp laikini yote ni maudhui. Kinachokuja kutofautisha kati ya maudhui mengi yanayoandikwa kila siku mtandaoni ni aina na stadi za uandishi. Nichukulie mfano wa mchekeshaji maarufu nchini, Idris Sultani, kuna wakati huandika posts kwenye ukurasa wake wa instagram akitangaza makampuni kama Uber. Uandishi wake ni mwepesi n wenye ucheshi, lakini hapo ameweza kutangaza biashara.

Kwa makampuni na taasisi mbalimbali unaweza kuajiri muandaa maudhui na mwongozaji wa akaunti za kijamii za kampuni. Tanzlyt ni kampuni inayotoa huduma kama hizi kwa makampuni na taasisi mbalimbali. Wanao wataalamu waliobobea katika masuala ya ‘digital marketing’ ikiwa ni pamoja na masuala ya uendeshaji mitandao ya kijamii, uandaaji wa ripoti na newsletters, utengenezaji wa tovuti na kadhalika

Kuna mbinu nyingi za uandishi kulingana na aina ya huduma au kampuni hivyo hata lugha inatakiwa itumiketofauti. Lakini unapotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii jitahidi kutumia lugha ambayo kila mtu ataelewa. Hata yule ambaye hakumaliza kidato cha nne angalau apate mwanga wa nini unazungumzia. Usiandike kama unaenda kusahihishwa na profesa wa lugha chuoni.